Kwa uongozi na mchango mkubwa wa Maulana Sayyid Arifu Naqawi, Hujjatul Asr Society of Tanzania iliandaa na kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) katika kituo cha Hawzat Imam Ridhwa (A.S).

15 Septemba 2025 - 18:54

Maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) Yafanyika kwa Mafanikio Tanzania +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- tarehe: 14 Septemba 2025 - 1446 Hijiria - Kituo cha Hawzat Imam Ridhwa (A.S) kilichopo Ikwiriri - Tanzania kimefanya Hafla adhimu ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (saww), Hafla iliyoandaliwa na Hujjatul Asr Society of Tanzania chini ya usimamizi wa Maulana Sayyid Arifu Naqawi (Mwenyezi Mungu amuhifadhi).

Maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) Yafanyika kwa Mafanikio Tanzania +Picha

Shughuli Zilizofanyika

Katika sherehe hizi, waumini walishiriki kwenye shughuli mbalimbali zenye hamasa na mafunzo, zikiwemo:

  1. Usomaji wa hadithi na mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) kwa wanafunzi wa madrasa.
  2. Ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani yao.
  3. Hotuba ya Maulid iliyoangazia nafasi ya Mtume (saww) katika kujenga jamii bora.
  4. Ukataji wa keki kama ishara ya kumuenzi na kumkumbuka Mtume Muhammad (saww).
  5. Shughuli nyingine za burudani na ibada zinazohusiana na Maulid pia zilichukua Nafasi muhimu katika Hafla hii.

    Maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) Yafanyika kwa Mafanikio Tanzania +Picha

    Ujumbe wa Maulana Sayyid Arif Naqvi 

Baada ya shughuli, Maulana Sayyid Arif Naqvi alitoa nasaha kwa wanafunzi na walimu. Alisisitiza nidhamu na maadili, akibainisha kuwa nidhamu ndiyo msingi wa kujenga jamii yenye staha na inayoongozwa na mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W.W).

Maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) Yafanyika kwa Mafanikio Tanzania +Picha

Mwisho 

Sherehe za Maulid zilifanyika kwa utulivu na mafanikio makubwa, zikionyesha mshikamano na mapenzi makubwa ya Waumini kwa Mtume Muhammad (saww).

Your Comment

You are replying to: .
captcha